Posts

Showing posts from April, 2024
Image
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni Dodoma Aprili 29, 2024, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na makadirio ya Bajeti ya mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2024/2025. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA  MSIMAMIZI MKUU  KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 0754264203

DKT NCHIMBI ALIVYOSISITIZA SUALA LA MBOLEA, KUDUMISHA UPENDO NA MSHIKAMANO

Image
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Nchimbi akihutubia wananchi katika ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa, amesisitiza serikali  kusambaza  mbolea kwa wakati na kutafuta masoko ya mazao ya wakulima lakini pia amewaomba watanzania kudumisha upendo na mshikamano kwa mstakabali wa utulimu na usalama wa nchi. Katika ziara hiyo ya siku 10 katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya , Njombe na  kuhitimishwa mkoani Ruvuma Aprili 23, 2024 yenye lengo la kukihuisha chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kutoa elimu juu ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama. Dkt Nchimbi ambaye kwa upande wangu mimi nilimuona ni mtu mwenye msimamo, mkweli na uhakika, katika ziara hiyo yenye mafanikio makubwa aliambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM,  Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Ga...