Posts

EVANCE KAMENGE AMPONGEZA RAIS SAMIA ALIVYOONYESHA MABADILIKO NDANI YA CCM

  Na Lydia Lugakila Kagera Mkulima na mchumi kutoka Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera Evance Emanuel Kamenge amesema kuwa Rais Samia ni kiongozi wa mfano na wa kupongezwa kwani ameleta MABADILIKO makubwa ndani ya Chama Chama Cha mapinduzi CCM kwani CCM ya sasa sio kama ya zamani. Kamenge ametoa kauli hiyo wakati Akizungumza na Waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa namna gani anavyokitazama chama hicho kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Kamenge amesema Chama Cha mapinduzi CCM kinampa faraja kubwa yeye kama kijana baada ya kuona Rais Samia anavyokiongoza kwa mabadiliko makubwa ikiwemo kurejesha nidhamu na msimamo mzuri. "Chama hiki kimewapa vijana nafasi ngazi za juu za chama na Serikali, chama kimetoa somo kwa vyama vyama vingine"amesema Kamenge. Kamenge ameongeza kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimekuwa kikisukuma agenda zake kwa vitendo na ni chama ambacho kimekataa na kimepinga rushwa ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kinapobaini wanachama wake na Vi...

Ijuka Omuka festival kuufufua upya Mkoa wa Kagera.

  Na Lydia Lugakila Bukoba Tamasha kubwa na la aina yake la utamaduni litakalopambwa na chakula cha kiasili pamoja na wasanii wakubwa lijulikanalo kama IJUKA OMUKA linatarajiwa kuzinduliwa Desemba 18,2024 Mkoani Kagera huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Dotto Biteko lengo likiwa ni kufufua  Mkoa huo upya. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Desemba 14,2024 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa alisema kuwa Tamasha la IJUKA OMUKA lenye maana ya *kumbuka nyumbani* ni la pili kufanyika Mkoani Kagera baada ya tamasha la kwanza kuwahi kufanyika Mwaka 2023 ikiwa ni kutokana na Mkoa huo kuwahi kusifika sana na baadae ukashuka ndo maana kumeanzishwa matamasha kama hayo ili kuufufua Mkoa huo na kuurudisha upya ikiwemo masuala ya  kiuchumi pamoja na kiutamaduni huku vyakula vya asili vya Mkoa huo vikionyeshwa na kuonjwa. "Mwaka huu tunafanya Tamasha la pili litakalowaunganisha wazawa na waishio ndani na nje ya Mkoa pia nje ya...

Takukuru Kagera kuchukua hatua dhidi ya Rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

  Na Lydia Lugakila Bukoba Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imesema haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote watakaojihusisha na vitendo vya Rushwa kabla ya uchaguzi wa Serikali za mitaa,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Kauli hiyo ya imetolewa na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Ezekia Sinkara wakati akiongea na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo Manispaa ya Bukoba ikiwa ni katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2024. Sinkala amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaendelea kutoa kutoa elimu kwa Wananchi pamoja na makundi mbali mbali ikiwemo viongozi wa Kisiasa kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila kuwepo vitendo vya Rushwa . " Sote tunatambua tunaelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27,2024 ambapo kwa sasa shughuli mbali mbali za mchakato huo zinaendelea hivyo hatutaki kuona wala kusikia wanaojihusisha na vitendo vya Rushwa...

Wanakijiji Karagwe Kunufaika na Kivuko cha Kisasa Ziwa Burigi

  Na Lydia Lugakila Karagwe Wananchi katika kata za Rugu na Nyakasimbi, pamoja na maeneo jirani katika wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wanatarajia kuondokana  na adha ya kuvuka Ziwa Burigi kwa mitumbwi isiyo salama.  Serikali, kupitia Wizara ya Ujenzi, imetangaza mipango ya kuleta kivuko cha kisasa kitakachorahisisha usafiri na kuboresha usalama wa wakazi wa maeneo hayo. Hayo yamebainika katika kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kilichofanyika katika ukumbi wa Angaza  Novemba 13,2024. Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innosent Bashungwa, ametangaza habari hiyo njema kwa wananchi. “Kwa muda mrefu wananchi wa kata hizi wamekuwa wakitumia mitumbwi kuvuka ziwa hili ili kufanya shughuli zao za maendeleo" alisema Waziri Bashungwa. Waziri Bashungwa alisema, Serikali imeona umuhimu wa kuleta kivuko cha kisasa ambacho kitahakikisha usalama na kurahisisha shughuli zao. Kuvuka kwa mitumbwi kumeonekana kuwa hatarishi, ambapo Wananchi w...

Utekaji watu sasa wahamia kwa wachungaji, makanisa.

  Na mwandishi wetu Licha ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. Samia Suluhu Hassan kuonya  Utekaji wa watu, Watoto wakiwemo wanafunzi Mkoani Dar es Salaam, hivi karibuni hali hiyo haijakoma ambapo hivi sasa  imehamia Wilaya ya Muleba Mkoani  Kagera ambapo Wachungaji na Makanisa yao wanatekwa wanapoabudu kanisani. Kwa Mujibu wa barua ya Malalamiko ya Wachungaji wa Jumuiya Ndogo ya Kanisa la Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania (BCT) ya  Juni 19,2024 iliyoelezwa kwa  OCD Muleba, imedai Polisi walihusika kusimamia utekaji huo wakiwa na mitutu ya bunduki. Gazeti hili limebaini Jumapili Julai 21, 2024 katika Kanisa la  Kabare lililopo Wilayani Muleba watu wapatao 15 walivamia Kanisa hilo na kutaka kumteka Mchungaji na Mwenyekiti wa Makanisa ya Baptist Jumuiya ndogo ya Muleba aitwaye Domisian Kabyemela hata hivyo watekaji walielemewa na baadhi yao akiwemo Adeliki Mutongole, Delius Kashaba, Gozibert Kunkolidi na Denisi Rajabu kuambulia kipigo ...

CHATANDA AMMWAGIA SIFA SOPHIA MWAKAGENDA

Image
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Shika Foundation, Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda kwa kuandaa kongamano kubwa la Wanawake wafanyabiasha wadogo wa mbogamboga na matunda wa Mkoa wa Dodoma lilofanyika hivi karibuni  kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
Image
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni Dodoma Aprili 29, 2024, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na makadirio ya Bajeti ya mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2024/2025. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA  MSIMAMIZI MKUU  KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 0754264203