Ijuka Omuka festival kuufufua upya Mkoa wa Kagera.
Na Lydia Lugakila Bukoba Tamasha kubwa na la aina yake la utamaduni litakalopambwa na chakula cha kiasili pamoja na wasanii wakubwa lijulikanalo kama IJUKA OMUKA linatarajiwa kuzinduliwa Desemba 18,2024 Mkoani Kagera huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Dotto Biteko lengo likiwa ni kufufua Mkoa huo upya. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Desemba 14,2024 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa alisema kuwa Tamasha la IJUKA OMUKA lenye maana ya *kumbuka nyumbani* ni la pili kufanyika Mkoani Kagera baada ya tamasha la kwanza kuwahi kufanyika Mwaka 2023 ikiwa ni kutokana na Mkoa huo kuwahi kusifika sana na baadae ukashuka ndo maana kumeanzishwa matamasha kama hayo ili kuufufua Mkoa huo na kuurudisha upya ikiwemo masuala ya kiuchumi pamoja na kiutamaduni huku vyakula vya asili vya Mkoa huo vikionyeshwa na kuonjwa. "Mwaka huu tunafanya Tamasha la pili litakalowaunganisha wazawa na waishio ndani na nje ya Mkoa pia nje ya...