Takukuru Kagera kuchukua hatua dhidi ya Rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Na Lydia Lugakila Bukoba Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imesema haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote watakaojihusisha na vitendo vya Rushwa kabla ya uchaguzi wa Serikali za mitaa,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Kauli hiyo ya imetolewa na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Ezekia Sinkara wakati akiongea na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo Manispaa ya Bukoba ikiwa ni katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2024. Sinkala amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaendelea kutoa kutoa elimu kwa Wananchi pamoja na makundi mbali mbali ikiwemo viongozi wa Kisiasa kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila kuwepo vitendo vya Rushwa . " Sote tunatambua tunaelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27,2024 ambapo kwa sasa shughuli mbali mbali za mchakato huo zinaendelea hivyo hatutaki kuona wala kusikia wanaojihusisha na vitendo vya Rushwa...