DKT NCHIMBI ALIVYOSISITIZA SUALA LA MBOLEA, KUDUMISHA UPENDO NA MSHIKAMANO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Nchimbi akihutubia wananchi katika ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa, amesisitiza serikali  kusambaza  mbolea kwa wakati na kutafuta masoko ya mazao ya wakulima lakini pia amewaomba watanzania kudumisha upendo na mshikamano kwa mstakabali wa utulimu na usalama wa nchi.

Katika ziara hiyo ya siku 10 katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya , Njombe na  kuhitimishwa mkoani Ruvuma Aprili 23, 2024 yenye lengo la kukihuisha chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kutoa elimu juu ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama.

Dkt Nchimbi ambaye kwa upande wangu mimi nilimuona ni mtu mwenye msimamo, mkweli na uhakika, katika ziara hiyo yenye mafanikio makubwa aliambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM,  Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.



IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MHARIRI

BLOG YA TAIFA YA CCM

0754264203


 

Comments

Popular posts from this blog

Utekaji watu sasa wahamia kwa wachungaji, makanisa.

Takukuru Kagera kuchukua hatua dhidi ya Rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

CHATANDA AMMWAGIA SIFA SOPHIA MWAKAGENDA