Utekaji watu sasa wahamia kwa wachungaji, makanisa.
Na mwandishi wetu Licha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. Samia Suluhu Hassan kuonya Utekaji wa watu, Watoto wakiwemo wanafunzi Mkoani Dar es Salaam, hivi karibuni hali hiyo haijakoma ambapo hivi sasa imehamia Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo Wachungaji na Makanisa yao wanatekwa wanapoabudu kanisani. Kwa Mujibu wa barua ya Malalamiko ya Wachungaji wa Jumuiya Ndogo ya Kanisa la Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania (BCT) ya Juni 19,2024 iliyoelezwa kwa OCD Muleba, imedai Polisi walihusika kusimamia utekaji huo wakiwa na mitutu ya bunduki. Gazeti hili limebaini Jumapili Julai 21, 2024 katika Kanisa la Kabare lililopo Wilayani Muleba watu wapatao 15 walivamia Kanisa hilo na kutaka kumteka Mchungaji na Mwenyekiti wa Makanisa ya Baptist Jumuiya ndogo ya Muleba aitwaye Domisian Kabyemela hata hivyo watekaji walielemewa na baadhi yao akiwemo Adeliki Mutongole, Delius Kashaba, Gozibert Kunkolidi na Denisi Rajabu kuambulia kipigo ...