Takukuru Kagera kuchukua hatua dhidi ya Rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Na Lydia Lugakila
Bukoba
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imesema haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote watakaojihusisha na vitendo vya Rushwa kabla ya uchaguzi wa Serikali za mitaa,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Kauli hiyo ya imetolewa na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Ezekia Sinkara wakati akiongea na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo Manispaa ya Bukoba ikiwa ni katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2024.
Sinkala amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaendelea kutoa kutoa elimu kwa Wananchi pamoja na makundi mbali mbali ikiwemo viongozi wa Kisiasa kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila kuwepo vitendo vya Rushwa .
" Sote tunatambua tunaelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27,2024 ambapo kwa sasa shughuli mbali mbali za mchakato huo zinaendelea hivyo hatutaki kuona wala kusikia wanaojihusisha na vitendo vya Rushwa" alisema Naibu Mkuu huyo.
amewahimiza Wananchi wenye sifa kutumia haki yao kikatiba kujiandikisha na kupiga kura lakini pia kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi wa Serikali za mitaa huku akiahidi wala Rushwa kukiona cha moto.
Aidha amechukua nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Wananchi wa Mkoa wa Kagera wanaoendelea kuwapatia ushirikiano huku akiwaomba kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanakuwa na Kagera isiyo na Rushwa na kutimiza wajibu wao wa kukataa Rushwa na kutoa taarifa za vitendo hivyo.
Hata hiyo Taasisi hiyo imesaidia kuzuia Rushwa kwa kurejeshwa kwa ekari 8 za ardhi katika Kijiji cha Bugango kata ya Kakunyu Wilayani Misenyi Mkoani humo eneo ambalo lilikuwa limemilikishwa na mtu kinyume na makubaliano, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 18, na kubaini miradi 10 Kati ya 18 yenye thamani ya bilioni 3.137 kuwa na mapungufu yaliyohitaji marekebisho sawa na asilimia 55.55 ya miradi iliyofuatiliwa, uchambuzi wa mifumo miwili, utekelezaji wa programu ya Takukuru rafiki, Uelimishaji umma,uchunguzi na Mashtaka ambapo wamepokea jumla ya malalamiko 115.
Comments
Post a Comment